Saturday, 22 July 2017

MWENYEKITI WA CCM BOKORANI AIOMBA SERIKALI IMUWAJIBISHE TUNDULISU

:::::::NATAMANI KUONA TUNDU LISSU AKITUMIKIA ADHABU YA KIFUNGO JELA:::::::::::::

👉Nimesikia Jana kuwa Yule Msema Hovyo Ndg Lissu Kakamatwa akiwa uwanja wa Ndege wa JNIA akisafiri.

👉Nasema Asante sana Jeshi la Police Tanzania kwa Kazi Nzuri Hii! Hatuwezi Kuwa na Taifa la Mavuvuzela wa Kukwamisha Utendaji kazi kwa Kila Sekta na Idara kushutumu kukejeli na kupotosha mambo. Tunahitaji Kusikia Maneno ya Kushawishi na kuhamasisha Utendaji Kazi kwa walio na Kazi na wasio na Kazi, Kuhamasishwa Kujiajili au kutafuta Vibarua na kazi ili kujipatia mapato na Kuzungusha Pesa kwa Maisha yao ya Kila siku na Mwisho Kulipa Kodi nakuipatia Serikali mapato kushirikiana na kufanya Maendeleo ktk Taifa letu.

👉Leo Tundu Lissu Kawa Mpiga Kelele na Mtu wakuponda Jitihada za Rais na Maendeleo ya Serikali kila Kona, Lakini kawa Mchochezi na Mtu wa Maneno ya Kejeli na Matusi ndani na Nje ya Nchi, Ifikie mahala Taifa la Tanzania liwe lenye Wananchi wenye Hekima na Busara ambao Hujadili Hoja na sio Vihoja. Na hili tutafanikiwa kama Viongozi wetu bila Kujali Itikadi watakuwa na Nidhamu na Kushika Maslai ya Taifa na sio Vyama vyao na vyeo.

👉Natamani Kuona Tundu Lissu Akichukuliwa hatua kali za Kisheria dhidi yake na Iwe Funzo kwake na Wanaomshauri na Kushabikia Ujinga wake wajue kuwa Tanzania Mpya haitokuwa na Mafanikio kama Nchi haitakuwa na Wananchi wenye Nidhamu.

👉Mataifa ya Wenzetu yaliyoendelea Hawana Watu wa Hovyo kama tulionao hapa kwetu kama huyu .... ambao kazi yao nikuponda tu na Kupanda Mbegu za Mawazo Hasi kwa Jamii yetu.

👉China imefikia Pale Ilipo nikwasababu kila Mmoja ilimlazimu kuishi kwa Nidhamu na kufuata Sheria, Taratibu, Kanuni na Miongozi walojiwekea kwa Faida ya Taifa zima, Uhuru Wanao usiozidi Mipaka.
Hawa Kina Lissu Wanataka Uhuru Usio na Kikomo HAIWEZEKANI.

👉Tunapokwenda katika Mabadiliko na Mapinduzi Makubwa ya Kiuchumi na Mfumo Lazima Wananchi tuwe na Mlengo Chanya nakushikamana sio Kuyumbishwa na Wanasiasa wanaokoswa na Hekima na Busara.

👉Juzi Lissu Kalopoka Maneno ya Ajabu kabisa alipokuwa na Waandishi. Kwa Tabia kama Hizi ndio maana Kuna Mataifa Hutoa Adhabu ya Kuwalipua Baadhi ya Wajinga wajinga kwa Mabomu tena katika Uwanja wa Mpira kila Mmoja Akishuhudia, TV, Radio na Magazeti Picha Kuoneshwa ili Ujinga huo usirudiwe na Mwingine.

👉VIJANA wenzangu Naomba Tupaze Sauti na Kukemea Tabia za Lissu kwani Anayoyafanya hayana Manufaa, Shibe wala Faida yoyote kwa Taifa zaidi ya Kutuharibia na Kutuponza tupate Shida ikiwa yeye anazo namna zakukimbia Nchini kama Taifa Litaingia Machafukoni atakuwa Huko kwa Wazungu wake alikotoka Juzi kati apa.

👉MAWAKILI na WANASHERIA wa Serikali pia Askari Polisi Emu tutumie Vifungu Ipasavyo ili isionekane kama ni Mchezo wa Kamata Achia Kamata achia kwa LISSU.
Ifikie Mahala Lissu atumikie Adhabu kwa Ujinga na Upuuzi wake wa Kila siku, Bila Kujali Hivyo Vyeo vyake na Umaarufu wake kwani katika Taifa Hili Binadamu wote ni Sawa.

👉Kwa  anayozungumza kila siku nakutuharibia Vijana na Taifa hili Pia Tabia yakwenda Nje ya Nchi kujipendekeza nakutushitaki kwa Hao Wazungu ambao Miaka yote hawajawai kuwa Marafiki wakweli bila Kuwa na Faida na Jambo yeye anakwenda nakusema uwongo ili Wamsaidie kwa Lipi, Wazungu ndio Waje kutuamulia Mambo yetu?
Historia zinajieleza Mataifa yaliharibiwa vibaya kama Libya walikuwapo Watu kama kina Lissu walioshawishiwa nakudanganywa kwa Faida zao wakalighalimu Taifa mpaka Leo Libya Sio Taifa lakueleweka.

👉Nasema Lissu Apewe Adhabu ambayo Itakuwa Fundisho kwake na wenzake.

Nawasilisha ni YONA mkiti wa CCM tawi la bokorani.

0 comments:

Post a Comment

DataTz Group Tech

DataTz Group Tech
Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea BLOG, WEBSITE, LOGO, PHONE APP, vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762 Asante na Karibu Sana.