DIWANI MWINGINE WA CHADEMA AJIUZULU NA KUJIUNGA CCM ARUSHA LEO
Napenda Kutoa Taarifa Kwa Umma Wa Wananchi Wa Kata Ya Ngabobo Kuwa Aliyekuwa Diwani Wa Chadema Ndugu Solomon Laizer Amejiuzulu Leo Kwa Kuungana Na Serikali Ya Awamu Ya Tano Chini Ya Rais John Pombe Magufuli Kwa Kazi Nzuri Anayofanya Kwa Taifa.
Ndugu Solomon Laizer Anakuwa Diwani Wa Tano Kujiuzulu Wilayani Hapa Arumeru Mashariki Kwa Kuridhishwa Na Utendaji Na Uchapakazi Wa Rais Magufuli katika Kuwatumikia Wananchi Kwa Dhamira Njema Mintarafu Mapambano Ya Vita Vya Uchumi, Rushwa, Ufisadi, Ubadhirifu Wa Mali Za Umma, Kurudisha Nidhamu Kwenye Utumishi Wa Umma Na Kusimamia Uwajibikaji Kwa Rasilimali Za Nchi Ndio Masuala Mtambuka Aliyokuwa Anayopigania Toka Alipojiunga Na Chama Cha Chadema Hivyo Hana Budi Kujiunga Moja Kwa Moja Na Mh. Rais.
Mosi Diwani Solomon Laizer Anasema Kuwa Mkuu Wa Wilaya Ndugu Alexander Mnyeti Ni Miongoni Mwa Viongozi Waliomvutia Sana Na Kuamua Kujiuzulu Nafasi Yake Kutokana Na Uhodari Wa Utendaji Wake Kwa Kuchapa Kazi Nzuri Usiku Na Mchana Pasipo Kuangalia Masuala Ya Itikadi Za Vyama, kabila Wala Dini Kwa Kuweka Mbele Uzalendo (patriotism) Kwa Maendeleo Ya Wananchi Kwanza, Anakiri Wazi Kwa Sasa Arumeru Imebadilika Sana Kutokana Na Uwepo Wa DC Mnyeti Kwa Kusimamia Majukumu Yake Ipasavyo Pasipo Upendeleo Wowote Na Kuifanya Arumeru Kuwa Sehemu Salama Ya Kuishi Kwa Mfano Mdogo Vurugu Za Mashamba Kupungua, Utatuzi Wa Migogoro Ya Maji Kwenye Kata Yake Kwa Njia Ya Amani Na Hekima Sana Ni Sehemu Ya Utendaji Mzuri Sana Wa DC Mnyeti.
Aghalabu Diwani Solomon Laizer Anakiri Wazi Kuwa Kwa Sasa Chadema Pamoja Na Madiwani Wenzake Kwenye Wilaya Ya Arumeru Walikuwa Kikwazo Kikubwa Cha Migogoro Isiyokwisha Kwa Kutokusimamia Majukumu Waliyotumwa Na Wananchi Wao Na Kuweka Maslahi Yao Mbele Zaidi Kuliko Maendeleo Ya Wilaya Na Kuwa Sehemu Ya Kumkwamisha Miradi Mbalimbali Inayoletwa Na Serikali Kupitia Vikao Vyao Kwa Mantiki Hiyo Ameona Bora Akae Pembeni ili Kuungana Na Serikali Ya Awamu Ya Tano Ya Rais John Pombe Magufuli.
Akihitimisha Diwani Laizer Amewaomba Sana Wananchi Wake Wa Kata Ya Ngabobo Kwa Moyo mkunjufu Kumpa Ushirikiano Wa Karibu Mkuu Wa Wilaya Alexander Mnyeti Na Watendaji Wote Wa Serikali Katika Kuwaletea Maendeleo Yao Kwenye Kata Hiyo Kwani Anajua Uchungu Wa DC Mnyeti Juu Ya Changamoto Zinazowakabili Kwa Sasa Na Kwamba Ushirikiano Ndio Eneo La Msingi Kumaliza Hizo Changamoto Zilizobakia Kwa Sasa.
Diwani Solomon Laizer Amekabidhi Barua Zake Zote Kwa Maandishi Kwa Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Meru Na Ofisi Ya Mkuu Wa Wilaya Kama Kumbukumbu Sahihi Ya Kujiuzulu Kwake Leo Tarehe 10.07.2017
Asanteni.
Na Mwandishi.
Personal assistance of chairman
Tuesday, 11 July 2017
CHADEMA YAKIMBIWA
July 11, 2017
No comments
DataTz Group Tech
DataTz Group Tech
Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea BLOG, WEBSITE, LOGO, PHONE APP, vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762 Asante na Karibu Sana.
Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea BLOG, WEBSITE, LOGO, PHONE APP, vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762 Asante na Karibu Sana.
0 comments:
Post a Comment