Friday, 21 July 2017

JESHI LA POLISI LA UWA MAJAMBAZI WA KIBITI


Kupitia Taarifa ya Habari kwenye Televisheni za Tanzania leo July 20, 2017 zipo taarifa nyingi zimeripotiwa na moja kubwa ni kuhusu mapambano ya Polisi dhidi ya watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika operesheni maalum Kibiti, Pwani.
Taarifa hiyo ambayo imerushwa na Kituo cha Channel 10 ambapo wakati wa zoezi la kuwasaka wahalifu likiendelea Kibiti leo imeripotiwa kuwa Jeshi la Polisi limewaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu hao.
Mkuu wa Operation hiyo Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabaas amesema tukio hilo limetokea katika eneo la Utende lililopo Kata ya Ikwiriri Wilayani Rufiji baada ya Polisi kuwatilia shaka watu watano na walipowafuatilia walikimbia na kuwashabulia Askari kwa risasi na katika majibizano Askari walifanikiwa kuwajeruhi wawili ambao walifariki njiani wakati wanapelekwa Hospital ya Taifa Muhimbili.

0 comments:

Post a Comment

DataTz Group Tech

DataTz Group Tech
Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea BLOG, WEBSITE, LOGO, PHONE APP, vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762 Asante na Karibu Sana.