Ni kauli za mwenyekiti wa chama cha mapinduzi tawi la bokorani JOSEPH YONA
Ameyazungumza hayo baadaya ongezeko la madiwani wa chama cha chadema kuhamia ccm
Alisema CHADEMA ni chama ambacho nakijua si chama cha chenye mipango ya kumkomboa mwananchi Si chama chenye democrasia wala uhuru wa kuhoji wala kujieleza wala kukosoa ni chama chenye muundo tofauti na CCM kwani maamuzi yote yanafanywa na watu wachache na ndio maana wengi wanakimbia sababu hakuna uhuru wa kisiasa
Alisema CHADEMA inapaswa kupingwa na wananchi wote wapenda maendeleo wapenda Taifa kwani hawana mapenzi na maendeleo ya TAIFA aliongeza na kusema kuwa ni wakati wa TANZANIA kusonga mbele ni wakati wa TANZANIA kupiga hatua tunapaswa kumuunga mkono Rais wetu kipenzi mwenye kukesha na kupigania Tanzania mpya ya viwanda
WATANZANIA tuweke tofauti pembeni tulipiganie Taifa JPM ni binadamu kama sisi ana moyo na damu kama hatuta Muunga mkono tutamfanya awe mpweke tufahamu ya kuwa hatuna Rais Mwingine kwa sasa
WAPINZANI tunawapenda sana tunaomba hoja za kulijenga Taifa na kumkomboa Mwananchi wa Tanzania
Serikali tunaiomba iwashughulikie wanasiasa wote wenye kuleta siasa chafu za kuvuruga amani ya nchi bila kujali vyama wanavyo tokea ili kuleta usawa na haki katika taifa.
Alizungumza leo katika ofisi za chama cha mapinduzi Tawi la bokorani lililopo Kata ya Mtoni wilaya Temeke Jijini Dar es salaam
Joseph yona
Mwenyekiti ccm bokorani
0 comments:
Post a Comment