CCM TAWI LA BOKORANI

Hapa ni nyumbani kwetu wote

MWENYEKITI WA TAWI

Kiongozi bora kwa ustawi wa tawi

TAWI LA WANANCHI WOTE

Tawi ni watu na watu ndo sisi

MWENYEKITI WA TAWI

Kiongozi bora kwa ustawi wa tawi

TAWI LA WANANCHI WOTE

Tawi ni watu na watu ndo sisi

TANZANIA YETU

Magufuli kwa maendeleo

Saturday, 29 July 2017

ALICHOFANYIWA JOSEPH YONA HAKIKUBALIKI

Uongozi wa chama cha mapindu tawi la bokorani umelaani kauli za mwenyekiti wa CHADEMA chalinze MATHAYO TORONGEY mwenyekiti huyo wa chadema ametoa maneno ya kujigamba kwamba liletukio la kumteka JOSEPH YONA mwenyekiti wa chama cha mapinduzi january 3 mwaka 2013 yeye anahusika au anawajua wahusika walio mteka

Kupitia ukurasa wake wa facebook MATHAYO TORONGEY Amedai kuwa operation hiyo ilifanywa baada ya chama hicho kusema Joseph yona ni msaliti wao torongey  ni mwanachadema na na mwenyekiti wa chalinze

Katibu wa siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi tawi la bokorani GODFREY HINJUSON amesema hata kama JOSEPH YONA alifanyiwa tendo hilo akiwa CHADEMA kama chama wanalaani kauli za Mwenyekiti wa chadema MATHAYO TORONGEY nakutaka mamlaka husika kuchukua hatua dhidi yake

JOSOPH YONA aliye onyesha ukomavu wa kisiasa kwakuwa na na uwezo wakuhoji. Na kusimamia misingi ya sheria za utawala bora kitu ambacho kilimfanya ashindwe kuendelea na CHADEMA kwani CHADEMA haiendeshwi kwa misingi ya demokrasia mpka kupelekea viongozi wake na wanachama kukosa kauli dhidi ya chama chao

Kwa sasa joseph yona ni mwenyekiti wa tawi la ccm bokorani alikili kuwa ccm ni chama makini chenye kuwa na mikakati ya kuishi zaidi ya miaka Mia alienda mbali na kusema mchakato wa kumpta mwenyekiti wa tawi ccm ni mgumu kuliko mwenyekiti wa taifa Chadema

Najivunia kuwa Mwenyekiti wa  Tawi n nitawatumikia wana ccm na wananchi wote wa bokorani

CHADEMA YAKILI KUHUSIKA NA UTEKWAJI WA JOSEPH YONA


Kupitia ukurasawa wake wa facebook mwenyekiti wa CHADEMA challinze MATHAYO TORONGEY amekubali kuwa chama cha democrasia na maendeleo Ambacho siku zote kimekuwa kikilia majukwani kuomba dhamna kwa wananchi kupewa ridhaa ya kuongoza Taifa hili ambalo linajivunia tunu zake za amani upendo na mshikamano

JOSEPH YONA ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi tawi la bokorani ambae mitazamo yake chanya nyenye tija kwa Taifa na wananchi wa hali ya chini Alifanyiwa unyama huo akiwa MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)  WILAYA YA TEMEKE
Katika hali ya sinto fahamu alichukuliwa na kundi la watu ambao walikuwa hawajurikani na kupigwa kuteswa na kutupwa lakini kupitia Mwenyekiti wa chalinze swala hili linakuja na mitazamo tofauti JE? CHADEMA ni chama cha kisiasa au kijasusi?

Aidha Mwenyekiti wa Ccm tawi la bokorani kasema atakuja na tamko rasmi kufwatia na kauli za mwenyekiti wa chadema chalinze alisema nilicho fanyiwa ni kitendo cha ukatili razima nichukue hatua.

Lakini alipata wasaa wa kuwashauri wanasiasa wote nchi katika vyama vyote vya kisiasa kuto kuwa na uoga wa kuhoji pale wanapo ona uongozi wa vyama vyao hautendi haki wasikubali kuburuzwa nilipo kuwa chadema nilihoji na nilipinga ukiukwaji wa sheria sikufungamana na vitendo ambavyo niliona havina tija hata ccm nitasimamia haki naamini nilitendewa haya sababu ya kusimamia haki na sheria Naipenda Tanzania nalipenda Taifa langu


By

Chairman's personal assistance

Wednesday, 26 July 2017

Wagombea wa TFF wakamatwa na TAKUKURU.....Yupo Pia Mtangazaji wa Clouds

Wagombea katika nafasi mbalimbali za uchaguzi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wa soka wamekatwa na TAKUKURU kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa jijini Mwanza.

Miongoni mwa waliyokamatwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), Almas Kasongo, Shafii Dauda  ambaye pia ni Mtangazaji wa Clouds Media Group, Elias Mwanjale, Leonald Malongo, Effam Majinge, Osuri Kasuli, Richard Kayenzi, Lazack Juma pamoja na Kelvin Shevi.

Hayo amebainisha Msemaji wa Takukuru Ernest Makale na kusema waliwakamata watu hao kwa kuweka mitego sehemu wanazofanyia vikao vyao vya siri.

"Tumewakamata kwa sababu hiki siyo kipindi cha kampeni na dalili zote kwamba walikuwa hapa kwa ajili ya uchaguzi unaotarajiwa zilikuwa zipo wazi, kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa tumeona kuna viashiria vya rushwa, tukaweka mitego katika sehemu walizokuwa wanaendesha vikao vyao vya siri tukaweza kuwakamata", amesema Makale.

Pamoja na hayo Makale amesema watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana ila wanaendelea na uchunguzi wao endapo watakapopata ushahidi wa kutosha watafikishwa mahakamani.

NDUGAI AKUBALI WABUNGE 8 CUF

SPIKA wa bunge la Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amekubaliana na barua iliyotumwa na Mwenyekiti wa cha cha wananchi CUF Prof IBRAHIM LIPUMBA  kwa kuwafuta unachama wabunge 8wa chama hicho

Spika amesema kufwatia msimamo wa chama hicho kuwafuta uwanachama mabunge hao 8 wanapoteza vigezo vya kuwa wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Alisema spika Nachuka nafasi hii kuutaarifu Umma kuwa nafasi za wabunge hao zipo wazi




   TOA MAONI YAKO

KAULI YA JOSEPH YONA KUHUSU CHADEMA KUHAMIA CCM

Ni kauli za mwenyekiti wa chama cha mapinduzi tawi la bokorani JOSEPH YONA


Ameyazungumza hayo baadaya ongezeko la madiwani wa chama cha chadema kuhamia ccm

Alisema CHADEMA ni chama ambacho nakijua si chama cha chenye mipango ya kumkomboa mwananchi Si chama chenye democrasia wala uhuru wa kuhoji wala kujieleza wala kukosoa ni chama chenye muundo tofauti na CCM kwani maamuzi yote yanafanywa na watu wachache na ndio maana wengi wanakimbia sababu hakuna uhuru wa kisiasa

Alisema CHADEMA inapaswa kupingwa na wananchi wote wapenda maendeleo wapenda Taifa kwani hawana mapenzi na maendeleo ya TAIFA aliongeza na kusema kuwa ni wakati wa TANZANIA kusonga mbele ni wakati wa TANZANIA kupiga hatua tunapaswa kumuunga mkono  Rais wetu kipenzi mwenye kukesha na kupigania Tanzania mpya ya viwanda

WATANZANIA tuweke tofauti pembeni tulipiganie Taifa JPM ni binadamu kama sisi ana moyo na damu kama hatuta Muunga mkono tutamfanya awe mpweke tufahamu ya kuwa hatuna Rais Mwingine kwa sasa

WAPINZANI tunawapenda sana tunaomba hoja za kulijenga Taifa na kumkomboa Mwananchi wa Tanzania

Serikali tunaiomba iwashughulikie wanasiasa wote wenye kuleta siasa chafu za kuvuruga amani ya nchi bila kujali vyama wanavyo tokea ili kuleta usawa na haki katika taifa.

Alizungumza leo katika ofisi za chama cha mapinduzi Tawi la bokorani lililopo Kata ya Mtoni wilaya Temeke Jijini  Dar es salaam



Joseph yona
Mwenyekiti ccm bokorani

Sunday, 23 July 2017

WENGINE SONGWE WAKIMBIA


Ziara ya Kiongozi mkuu wa shughuli za selikari Waziri Mkuu KASSIMU MAJALIWA katika mkoa mpya wa songwe uliopo mipakani kabisa mwa Tanzania na Zambia na Malawi imefawafanya wananchi kuonyesha imani yao kubwa na Serikali ya chama cha Mapinduzi kupelekea wanachama zaidi ya mia tatu wa chama cha democrasia na Maendeleo CHADEMA kukiama chama hicho na kujiunga na CCM

Waziri Mkuu ambae alionyesha hali ya kuto kuwa na Uvumilivu na watendaji wa serikali ambao wapo katika maslai yao na si maslai ya Umma

Wanachama wa chama cha CHADEMA wamesema tumeona ni bora tuiunge mkono selikari ya JPM chini ya Ilani ya CCM

Mmja ya wanachama walio hamia CCM alisema chadema hakuna usawa na haki hivyo democrasia imekaliwa alienda mbali na kusema jimbo la vwawa mbunge wa viti maalum kupitia CCM ni mzawa wa wilaya ya Mbozi wanamfahamu toka akiwa si mbunge lakini CHADEMA mbunge wa viti maalum si mkazi wa Mbozi ni mtu wa KILIMANJARO hivyo alisema CHADEMA ni chama cha ubaguzi kinapaswa kukataliwa na wananchi wote

Aliomba Msamaha kwa matusi aliyo wahi kutukana selikari na viongozi wa ccm aliomba kurudi kwa baba na mama

Mkuu wa mkoa wa Lindi ambae pia ni Mwenyekiti wa ccm Mbeya na Songwe aliwapokea wanachama Hao Mbele ya Waziri Mkuu wa TANZANIA

SIASA CHAFU HAIVUMILIKI KAMANDA SIRO

Hatuta mvumilia mwanasiasa yeyote atakae fanya siasa chafu kwa ajiri y kujipatia umaarufu alisema hayo IGP SIRRO baada ya Kuwepo na mkundi ya wanasiasa wenye kutekeneza chuki ya wananchi kwa serikali

SITA WAVUMILIA

MAJALIWA AWASIMAMISHA WATUMISHI MBOZI


Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh MAJALIWA leo ame wasimamisha kazi watumishi wa umma wa wilaya ya mbozi iliyopo mkoa Mpya wa Songwe

Mh Waziri mkuu kamsimamisha kazi mkurugenzi kaimu mkurugenzi watumiahi idara ya fedha na watumishk idara ya manunuzi

Amesema wilaya ya mbozi ni moja ya wilaya inayo nuka rushwa na ufisadi amesema watu hao wako chini ya TAKUKURU mpka watakapo toa taarifa rasmi

Kazi hyo ya kuhakikisha watumishi hao wa Umma kusimamishwa imetokana na jitihada za mbunge wa jimbo la Vwawa Mh Hasunga wa chama cha mapinduzi ccm

Mbunge huyo makini ambae pia  ni mtaalamu wa mambo ya uchumi alisema hayuko tayari kuona fedha za wapiga kura wake wananufaika wachache na huo ni mwanzo

Alimaliza na kusema Mafisadi hawana nafasi katika mkoa mpya wa Songwe

Saturday, 22 July 2017

MWENYEKITI WA CCM BOKORANI AIOMBA SERIKALI IMUWAJIBISHE TUNDULISU

:::::::NATAMANI KUONA TUNDU LISSU AKITUMIKIA ADHABU YA KIFUNGO JELA:::::::::::::

👉Nimesikia Jana kuwa Yule Msema Hovyo Ndg Lissu Kakamatwa akiwa uwanja wa Ndege wa JNIA akisafiri.

👉Nasema Asante sana Jeshi la Police Tanzania kwa Kazi Nzuri Hii! Hatuwezi Kuwa na Taifa la Mavuvuzela wa Kukwamisha Utendaji kazi kwa Kila Sekta na Idara kushutumu kukejeli na kupotosha mambo. Tunahitaji Kusikia Maneno ya Kushawishi na kuhamasisha Utendaji Kazi kwa walio na Kazi na wasio na Kazi, Kuhamasishwa Kujiajili au kutafuta Vibarua na kazi ili kujipatia mapato na Kuzungusha Pesa kwa Maisha yao ya Kila siku na Mwisho Kulipa Kodi nakuipatia Serikali mapato kushirikiana na kufanya Maendeleo ktk Taifa letu.

👉Leo Tundu Lissu Kawa Mpiga Kelele na Mtu wakuponda Jitihada za Rais na Maendeleo ya Serikali kila Kona, Lakini kawa Mchochezi na Mtu wa Maneno ya Kejeli na Matusi ndani na Nje ya Nchi, Ifikie mahala Taifa la Tanzania liwe lenye Wananchi wenye Hekima na Busara ambao Hujadili Hoja na sio Vihoja. Na hili tutafanikiwa kama Viongozi wetu bila Kujali Itikadi watakuwa na Nidhamu na Kushika Maslai ya Taifa na sio Vyama vyao na vyeo.

👉Natamani Kuona Tundu Lissu Akichukuliwa hatua kali za Kisheria dhidi yake na Iwe Funzo kwake na Wanaomshauri na Kushabikia Ujinga wake wajue kuwa Tanzania Mpya haitokuwa na Mafanikio kama Nchi haitakuwa na Wananchi wenye Nidhamu.

👉Mataifa ya Wenzetu yaliyoendelea Hawana Watu wa Hovyo kama tulionao hapa kwetu kama huyu .... ambao kazi yao nikuponda tu na Kupanda Mbegu za Mawazo Hasi kwa Jamii yetu.

👉China imefikia Pale Ilipo nikwasababu kila Mmoja ilimlazimu kuishi kwa Nidhamu na kufuata Sheria, Taratibu, Kanuni na Miongozi walojiwekea kwa Faida ya Taifa zima, Uhuru Wanao usiozidi Mipaka.
Hawa Kina Lissu Wanataka Uhuru Usio na Kikomo HAIWEZEKANI.

👉Tunapokwenda katika Mabadiliko na Mapinduzi Makubwa ya Kiuchumi na Mfumo Lazima Wananchi tuwe na Mlengo Chanya nakushikamana sio Kuyumbishwa na Wanasiasa wanaokoswa na Hekima na Busara.

👉Juzi Lissu Kalopoka Maneno ya Ajabu kabisa alipokuwa na Waandishi. Kwa Tabia kama Hizi ndio maana Kuna Mataifa Hutoa Adhabu ya Kuwalipua Baadhi ya Wajinga wajinga kwa Mabomu tena katika Uwanja wa Mpira kila Mmoja Akishuhudia, TV, Radio na Magazeti Picha Kuoneshwa ili Ujinga huo usirudiwe na Mwingine.

👉VIJANA wenzangu Naomba Tupaze Sauti na Kukemea Tabia za Lissu kwani Anayoyafanya hayana Manufaa, Shibe wala Faida yoyote kwa Taifa zaidi ya Kutuharibia na Kutuponza tupate Shida ikiwa yeye anazo namna zakukimbia Nchini kama Taifa Litaingia Machafukoni atakuwa Huko kwa Wazungu wake alikotoka Juzi kati apa.

👉MAWAKILI na WANASHERIA wa Serikali pia Askari Polisi Emu tutumie Vifungu Ipasavyo ili isionekane kama ni Mchezo wa Kamata Achia Kamata achia kwa LISSU.
Ifikie Mahala Lissu atumikie Adhabu kwa Ujinga na Upuuzi wake wa Kila siku, Bila Kujali Hivyo Vyeo vyake na Umaarufu wake kwani katika Taifa Hili Binadamu wote ni Sawa.

👉Kwa  anayozungumza kila siku nakutuharibia Vijana na Taifa hili Pia Tabia yakwenda Nje ya Nchi kujipendekeza nakutushitaki kwa Hao Wazungu ambao Miaka yote hawajawai kuwa Marafiki wakweli bila Kuwa na Faida na Jambo yeye anakwenda nakusema uwongo ili Wamsaidie kwa Lipi, Wazungu ndio Waje kutuamulia Mambo yetu?
Historia zinajieleza Mataifa yaliharibiwa vibaya kama Libya walikuwapo Watu kama kina Lissu walioshawishiwa nakudanganywa kwa Faida zao wakalighalimu Taifa mpaka Leo Libya Sio Taifa lakueleweka.

👉Nasema Lissu Apewe Adhabu ambayo Itakuwa Fundisho kwake na wenzake.

Nawasilisha ni YONA mkiti wa CCM tawi la bokorani.

MWENYEKITI CCM BOKORANI AMUCHAMBUA ZITO KABWE

:::::::Narudia::::::Huyu ndiye ZITTO ninayemfahamu::::::::

👉Sijawahi kuwa Mwanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo na sijafikiria kujiunga na chama hicho,japo nilishiriki kukianzisha. Nilishawahi kuwa Mwanachama wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) aka Nyumbu.

👉Nikiwa ndani ya CHADEMA nimewahi shiriki katika harakati nyingi zote zikiwa na lengo la kukikuza chama ambacho niliamini ndo mkombozi wa kweli wa mtanzania.

👉Bahati mbaya sikuwa sahihi, nilikosea kukiamini chama hicho ambacho idadi kubwa ya viongozi wake ni mahafidhina,wahuni,wasaniii.

👉Nikiwa ndani ya siasa, nimefanikiwa kujuana na wanasiasa wengi wakubwa kwa wadogo, mmoja wao ni kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.

👉Namjua Zitto, nafahamiana naye vizuri, ni mmoja wa wanasiasa wasomi, wenye siasa safi ambaye mara zote kauli na hoja zake zimetaliwa na busara na nia ya kulijenga taifa, siwezi kusema si mbinafsi moja kwa moja lakini nina imani nae kubwa kuwa si mbinafsi.

👉Zitto ameweza kuzimudu siasa safi na siasa taka zilizokuwa zikiendeshwa ndani na nje ya chadema kabla ya kuhamia ACT- Wazalendo.Ameweza kupambana na kupenya kwenye changamoto nyingi za kisiasa hasa siasa hizi za kuwa na chama kimoja kikongwe na chenye nguvu nchini na nje ya nchi.

👉Sote tunaijua CCM ni chama chenye wanachama na viongozi wanaoijua siasa, wanaweza kukibadili chama hicho wakati wowote, chama hiki kikuu nchini ni kama kinyonga, kinabadiilika kulingana na mazingira na wakati.

👉CCM kinapanga vyema karata zake, kina propaganda zenye kuwiana na ukweli tofauti na ilivyo kwa upinzani ambao wanadanganya wananchi mpaka wanajidanganya wao wenyewe.

👉Zitto ameweza kupenya kote huku na ndio maana leo hii, Zitto anaposulubiwa hata CCM kinaumia na kumhurumia, kwa sababu wanamjua mwanasiasa huyu kijana ni mtu wa namna gani.

👉Kama si uimara wa Zitto huenda angeshaanguka maana wapo watu na vyama vilivyotupwa nje ya siasa kutokana na kukosa misingi ya mapambano ya siasa za aina zote.

👉Hata hivyo chadema kimefika hapo kilipo pamoja na mambo mengine mchango wa Zitto unahusika kwa kiwango kikubwa.

Katibu mkuu wa zamani wa chadema Dr. Wilbroad Slaa kwa kushirikiana na Zitto walieweza kukifikisha chama hapo kilipo, hilo haliepukiki na anayekataa ana chuki zake binafsi.

👉Zitto akiwa mchanga kisiasa lakini mwenye maono alichanga karata zake vyema, akashiriki kukitoa chama kutoka kuwa na wabunge 11 hadi kukifikisha hapa kilipo, ambapo leo Kina wabunge wengi.

👉Historia ya Chadema haiwezi kukamilika bila ya kumhusisha Zitto katika mafanikio yake huku akipambana kwa karibu sana na Dr. Slaa, na mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye kwa bahati mbaya amejikuta akivurugwa na wapambe.(Yaani Halima Mdee yule binti Makini leo anatafuta Sifa za kitoto)

👉Chadema ya Zitto akiwa kama Naibu katibu mkuu Bara, waliweza kukidhibiti CUF ya enzi za Hamad Rashid ambaye alikuwa kinara ndani ya bunge.

👉CUF ilikuwa na hoja dhaifu na mikakati isiyotekelezeka pamoja na kauli mbiu za hatari za mapanga shaa,Interehamwe na Saigon.nk

👉Chadema ya Zitto na Dr Slaa walikuwa wakitoa hoja zenye mashiko, walikuwa moto mkali ndani ya bunge, hakuna aliyeacha kuwasikiliza watu hao wanapopata nafasi ya kuzungumza.Bunge la 9 lilikuwa ni moto wa kuotea mbali.

👉Bunge hilo lilileta mapinduzi makubwa ya kiungozi na kiutendaji serikalini.Mikataba mibovu ilichambuliwa,Sakata la EPA iliiibuka, mgodi wa Buzwagi nao ulipewa nafasi na masikini walipiganiwa.

👉Chama kikanawiri na kushamiri hadi kufikia leo kuwa na wabunge wengii ajabu ni kwamba baadhi ya viongozi wa chama hicho wamesahau mema yote ya Zitto badala yake walishiriki kwenye harakati chafu za kumchafua na wanaendelea kumchafua.

👉Bahati mbaya Zitto kwa uungwana wake Kuna Muda anawahurumia Nyumbu anageuka kuwa kuwa Punda wa madawa wa mkwepa kodi Mkuu ambaye ni mwizi wa ruzuku ya chadema.

👉Wanataka kuiaminisha jamii kuwa Zitto ni Msaliti, kwamba anapaswa kutukanwa, kusimangwa na kubezwa. Zitto huyu anayejua kupanga karata leo hii amekuwa adui na msaliti wa chadema, chama alichojiunga nacho akiwa kinda!

👉Dhambi hii ya ubaguzi waliyoifanya Chadema itawarudia, hawatapona kamwe, hawatabaki salama, wataparanganyika tu, nawaombea heri wasifike huko ingawa dhambi ya ubaguzi haiishi.

👉Kama nilivyotangulia kusema hapo juu, namjua Zitto, nimefanya nae kazi ni mmoja wa waliokuwa viongozi kipenzi cha watu wa rika na kada zote ndani ya chama hicho.

👉Alipendwa naa viongozi wa ngazi ya chini Chadema, alikuwa ni mtu wa kujishusha na kuwasikiliza viongozi waliochini yake.Hata kama aliyoelezwa yalikuwa nje ya uwezo wake hakuyapuuza.

👉Tofauti yake na viongozi wakubwa wa chadema, yeye alikuwa akifika kwenye mikutano hata akute watu wachache hakuwa akiacha kuhutubia na kuwapa moyo.

👉Alikuwa akiyatumia mazingira hayo ya watu wachache kusimulia baadhi ya visa vyake vya kisiasa, wakati huo ndo wanajenga chama.

👉Naamini anakikumbuka kisa hiki, kwamba yeye ZITTO na Halima Mdee wa zamani walikwenda mahali na kukuta watu wachache.Hawakuacha kuhutubia, walihutubia, lakini ajabu hao watu wachache waliokuwepo walikuwa wakiendelea na harakati zao, wengi wao walikuwa wakinunua ndizi mbivu......Kwa maana nyingine hawakuwa wakisikilizwa.

👉Alichokifanya ni kumuomba Mdee akazinunue zile ndizi zote ili watu wakose cha kununua na badala yake wageuke kuwasikiliza.

👉Hata hivyo, mpango wao huo haukufanikiwa, kwani kila mtu aliyekuwa pale aliendelea na mambo yake.
Chakufurahisha Zitto na Mdee wa zamani hawakukata tamaa, walipambana kuwashawishi watu wakielewa chama.Leo hii chama kikifika eneo lile lile watu wanakanganyana ili kumsikiliza kiongozi wa chama anayezungumza hata kama anaongea pumba.

👉Zitto alikuwa mtu wa kujichunga sana katika matamshi yake, hakuwa akiongea bora aongee, alikuwa akiongea yanayopaswa kuongelewa kwa wakati huo na kwa wakati stahiki.


Na Ndo maana Kuna Muda Zitto akiongea Pumba namsamehe Kwa kuwa naamini ni mwanadamu kosa Moja si kosa.

👉Leo Zitto Huyu Moja ya wanasiasa niliye na imani ninapomuona anafanya harakati za kimaendeleo na rais wa awamu ya tano niliyemuota tokea nikiwa mdogo nasikia Faraja sana.

👉Mwisho ZITTO usikate tamaa songa mbele Utafika,hallow Zitto jaribu kurudia historia ya rafiki yako aliyekuwa rais wa CHINA Zamani Deng Xiao Ping utamuelewa Dr Magufuli.

Nawasilisha ni YONA mkiti wa CCM tawi la bokorani.
 ( 0713802226)

Friday, 21 July 2017

WAZIRI MKUU AWASHA MOTO MKOA WA SONGWE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amempa miezi miwili kuanzia leo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe, Elias Nawera abadili mwenendo wake kiutendaji na ashirikiane vizuri na Mkuu wa wilaya hiyo Samwel Jeremiah.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Alhamisi hii, wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Songwe akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Songwe.
Amesema watumishi wote wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi yaweze kufikiwa. Pia waheshimiane sehemu za kazi na kila mtu azingatie mipaka ya madaraka yake.
“Mkurugenzi hapa hamsikilizi Mkuu wa wilaya anaondoka kituo cha kazi bila ya kuaga na amewagawa wakuu wa Idara. Namtaka afanye mabadiliko ya utendaji wake ndani ya miezi miwili na Mkuu wa Mkoa fuatilia jambo hili,” alisisitiza Waziri Majaliwa.
Pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote wasimamie utendaji wa wakurugenzi wa Halmashauri kwenye maeneo yao ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo.”Serikali hii si ya mchezo. Serikali hii inahitaji watumishi waadilifu wa kuwatumikia Watanzania.”
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Bibi Chiku Galawa amesema wamejipanga kuhakikisha changamoto zote zinazoukabili mkoa zinaboreshwa pamoja na kufikia malengo ifikapo 2020

JESHI LA POLISI LA UWA MAJAMBAZI WA KIBITI


Kupitia Taarifa ya Habari kwenye Televisheni za Tanzania leo July 20, 2017 zipo taarifa nyingi zimeripotiwa na moja kubwa ni kuhusu mapambano ya Polisi dhidi ya watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika operesheni maalum Kibiti, Pwani.
Taarifa hiyo ambayo imerushwa na Kituo cha Channel 10 ambapo wakati wa zoezi la kuwasaka wahalifu likiendelea Kibiti leo imeripotiwa kuwa Jeshi la Polisi limewaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu hao.
Mkuu wa Operation hiyo Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabaas amesema tukio hilo limetokea katika eneo la Utende lililopo Kata ya Ikwiriri Wilayani Rufiji baada ya Polisi kuwatilia shaka watu watano na walipowafuatilia walikimbia na kuwashabulia Askari kwa risasi na katika majibizano Askari walifanikiwa kuwajeruhi wawili ambao walifariki njiani wakati wanapelekwa Hospital ya Taifa Muhimbili.

Thursday, 20 July 2017

CCM HAIWEZI KUTOKA MADARAKANI



Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi tawi la bokorani YONA JOSEPH amesema chama cha mapinduzi ni chama makini chenye mikakati ya kuishi zaidi ya miaka mia hivyo itakuwa vigumu kutoka madarakini

Lakini pia alisema udhaifu wa wapinzani tamaa za madaraka kujilimbikizia mali mahitaji ya mtu mmja mmja ya wapinzani wanazidi kuwa imanisha wananchi kwamba hakuna maendeleo nje ya chama chamapinduzi

Alizidi kusema kuwa ni wakati wa watanzania wote sasa kumuunga mkono rais JPM kwani anania ya dhati ya kuwatumikia wananchi

Mwenyekiti huyo ambae kwasasa anaendeleza operation yke ya CCM KARIBU NYUMBANI WANANCHI TUSOME UHURU amesema kwamba wanachi wote ni wakati wa kupinga vikali vyombo vya habari vinavyo toa habari za uchochezi na ugombanisha hivyo kuwataka wananchi kusoma gazeti la uhuru kwani ni lenye tija kwa umma


By

Chairman's personal assistance

Monday, 17 July 2017

DIWANI WA CHADEMA APEWA DHAMANA

Baada ya kushitakiwa kwa kesi ya kuomba rushwa

HAKUNA DEMOCRASIA YA KWELI NDANI YA UKAWA



Mwenyekiti wa ccm tawi la bokorani Mh JOSEPH YONA  ameyasema hayo juzi alipo kuwa akiongea na waandishi gazeti la uhuru na mzalendo mwenyekiti huyo ambae sasa amekuwa na mitazamo chanya ya kukijenga chama cha mapinduzi kupitia tawi la bokorani lililopo Kata ya Mtoni wilaya ya Temeke mkoa Wa Dar es salaaam

Mwenyekiti wa ccm amesema kuwa hakuna democrasia ya kweli ndani ya ukawa hivyo kupelekea umoja huo kuto kuwa na tija wala manufaa kwa Taifa

Alisema kunaukandamizaji ndani ya ukawa CHADEMA wanaleta ubebari kwa vyama vingine mpka kupelekea vyama hivyo kuwa na migogoro ya ndani ya chama

Amesema na ushangaa uongozi wa ukawa unasema serikali ya ccm haina democrasia ya kweli wakati ndio chama pekee kimekuwa na uchaguzi wa huru kuanzia ngazi ya tawi mpka taifa

Alimaliza na kusema kumekuwa na ongezeko kuu la wananchi kuwa na imani na serikali yake na kuwa taka wananchi wote kuumunga mkono rais na serikali katika kutekeleza sera na mikakati akinifu ya kulikomboa Taifa                                                                                                            

Saturday, 15 July 2017

MAGAZETI YA LEO JULAI 15,2017





DD





Mahakama Yakataa Ombi la Kigogo wa Escrow Harbinder Singh Seth Kutibiwa Nje ya Nchi

SERIKALI YA MAGUFULI HAITAKI MCHEZO WALI TULALIA LALIA SASA ZAMU YETU KUWALALIA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa ombi la Mawakili wanaomtetea mfanyabiashara Harbinder Singh Seth la kumruhusu mteja wao kwenda nje ya nchi kutibiwa uvimbe uliopo tumboni na badala yake apatiwe tiba kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili. 

Wakili wa kujitegemea, Alex Balomi aliifahamisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana kuwa Harbinder Singh Sethi anaumwa, hali yake imeendelea kubadilika na hii  ni wiki ya nne sasa  hawezi kupata usingizi.

Wakili Balomi aliiambia mahakama hiyo kuwa Sethi anasumbuliwa na uvimbe tumboni ambao unahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari.

“Kutokana na hali yake kuwa mbaya hii ni wiki ya nne sasa hawezi kupata usingizi hivyo anahitaji  ungalizi wa karibu wa madaktari  na kwamba wamebahatika kupata nyaraka kadhaa kutoka kwa daktari,”Balomi  aliifahamisha mahakama. 

Balomi aliongeza kuwa hata siku aliyokamatwa alikuwa akienda kwenye matibabu Afrika Kusini.

Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Leonard Swai  alisema  nyaraka ambazo Wakili Balomi anataka kuziwasilisha mahakamani hapo kuhusiana na Sethi hazijakidhi vigezo vya kisheria  na kwamba alitegemea daktari ambaye anamtibu angefika mahakamani kueleza hali  halisi ya ugonjwa husika.

Kutokana na hoja hizo,  Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alisema suala la ugonjwa si la kufumbiwa macho, linapaswa kuchukuliwa kwa uzito na kuelekeza magereza kufanya kila linalowezekana kuhakikisha hali ya mshtakiwa huyo inabaki katika hali nzuri na inapobidi wawasiliane na wataalam wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kesi imeahirishwa hadi Julai 28, 2017 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Katika kesi hiyo, Sethi na James Rugemalira wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola 22, 198,544.60 sawa na Sh 309,461,300,158.27.

Thursday, 13 July 2017

MPASUKO UKAWA

Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ambao uliundwa na vyama vya upinzani ktk kushughulikia katiba mpya umejikuta kuwa na wakati mgumu na kuwafanya wananchi kukosa imani na ummoja huo hayo yalijidhilisha sana katika uchaguzi  Mkuu wa 2015 kwa kile kilichodaiwa ni uchu wa MADARAKA na maslai ya chama kimoja kimoja kuwa mbele na kuuacha ummoja huo bila muelekeo mzuri

Aidha kaimu katibu mkuu wa chama cha wanainchi (CUF) Bi Magdalena sakaya  amewatuhumu baadhi ya wabunge wa chama cha chadema na kusema wamekuwa wakichangishana pesa ili kuwapa watu wafanye vurugu ionekane kuna vurugu ndani ya chama cha CUF

Imepelekea kaimu huyo kutangaza vita vikali dhidi ya CHADEMA maana imebaini ndio chanzo cha migogoro yao

Bi magdalena aliongeza na kusema kuwa CUF nichama na si taasisi ya mtu binafsi hivyo inauongozi wake kwa mujibu wa katiba hivyo hawako tayari kuona kina vurugwa na CHADEMA

Alisema kuna mipango ya kuhujumu chama chetu inayofanyawa na washiriki wa SEIF SHARIF HAMAD NA CHADEMA kwa kuwa kusanya vijana wahuni kutoka mabibo manzese tandika na vingunguti kwaajiri ya kuwapeleka mahakamani kuwa dhurumu viongozi wa chama


TOA MAONI YAKO

Tuesday, 11 July 2017

CHADEMA YAKIMBIWA

DIWANI MWINGINE WA CHADEMA AJIUZULU NA KUJIUNGA CCM ARUSHA LEO Napenda Kutoa Taarifa Kwa Umma Wa Wananchi Wa Kata Ya Ngabobo Kuwa Aliyekuwa Diwani Wa Chadema Ndugu Solomon Laizer Amejiuzulu Leo Kwa Kuungana Na Serikali Ya Awamu Ya Tano Chini Ya Rais John Pombe Magufuli Kwa Kazi Nzuri Anayofanya Kwa Taifa. Ndugu Solomon Laizer Anakuwa Diwani Wa Tano Kujiuzulu Wilayani Hapa Arumeru Mashariki Kwa Kuridhishwa Na Utendaji Na Uchapakazi Wa Rais Magufuli katika Kuwatumikia Wananchi Kwa Dhamira Njema Mintarafu Mapambano Ya Vita Vya Uchumi, Rushwa, Ufisadi, Ubadhirifu Wa Mali Za Umma, Kurudisha Nidhamu Kwenye Utumishi Wa Umma Na Kusimamia Uwajibikaji Kwa Rasilimali Za Nchi Ndio Masuala Mtambuka Aliyokuwa Anayopigania Toka Alipojiunga Na Chama Cha Chadema Hivyo Hana Budi Kujiunga Moja Kwa Moja Na Mh. Rais. Mosi Diwani Solomon Laizer Anasema Kuwa Mkuu Wa Wilaya Ndugu Alexander Mnyeti Ni Miongoni Mwa Viongozi Waliomvutia Sana Na Kuamua Kujiuzulu Nafasi Yake Kutokana Na Uhodari Wa Utendaji Wake Kwa Kuchapa Kazi Nzuri Usiku Na Mchana Pasipo Kuangalia Masuala Ya Itikadi Za Vyama, kabila Wala Dini Kwa Kuweka Mbele Uzalendo (patriotism) Kwa Maendeleo Ya Wananchi Kwanza, Anakiri Wazi Kwa Sasa Arumeru Imebadilika Sana Kutokana Na Uwepo Wa DC Mnyeti Kwa Kusimamia Majukumu Yake Ipasavyo Pasipo Upendeleo Wowote Na Kuifanya Arumeru Kuwa Sehemu Salama Ya Kuishi Kwa Mfano Mdogo Vurugu Za Mashamba Kupungua, Utatuzi Wa Migogoro Ya Maji Kwenye Kata Yake Kwa Njia Ya Amani Na Hekima Sana Ni Sehemu Ya Utendaji Mzuri Sana Wa DC Mnyeti. Aghalabu Diwani Solomon Laizer Anakiri Wazi Kuwa Kwa Sasa Chadema Pamoja Na Madiwani Wenzake Kwenye Wilaya Ya Arumeru Walikuwa Kikwazo Kikubwa Cha Migogoro Isiyokwisha Kwa Kutokusimamia Majukumu Waliyotumwa Na Wananchi Wao Na Kuweka Maslahi Yao Mbele Zaidi Kuliko Maendeleo Ya Wilaya Na Kuwa Sehemu Ya Kumkwamisha Miradi Mbalimbali Inayoletwa Na Serikali Kupitia Vikao Vyao Kwa Mantiki Hiyo Ameona Bora Akae Pembeni ili Kuungana Na Serikali Ya Awamu Ya Tano Ya Rais John Pombe Magufuli. Akihitimisha Diwani Laizer Amewaomba Sana Wananchi Wake Wa Kata Ya Ngabobo Kwa Moyo mkunjufu Kumpa Ushirikiano Wa Karibu Mkuu Wa Wilaya Alexander Mnyeti Na Watendaji Wote Wa Serikali Katika Kuwaletea Maendeleo Yao Kwenye Kata Hiyo Kwani Anajua Uchungu Wa DC Mnyeti Juu Ya Changamoto Zinazowakabili Kwa Sasa Na Kwamba Ushirikiano Ndio Eneo La Msingi Kumaliza Hizo Changamoto Zilizobakia Kwa Sasa. Diwani Solomon Laizer Amekabidhi Barua Zake Zote Kwa Maandishi Kwa Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Meru Na Ofisi Ya Mkuu Wa Wilaya Kama Kumbukumbu Sahihi Ya Kujiuzulu Kwake Leo Tarehe 10.07.2017 Asanteni. Na Mwandishi. Personal assistance of chairman

Monday, 10 July 2017

KAULI NZITO ZA MWENYEKITI WA CCM BOKORANI

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi tawi la bokorani Mh JOSEPH YONA atoa kauli nzito kwa wana ccm wapinzani na wananchi wote Mheshimiwa huyo ambae ni takribani miezi miwili sasa toka ashinde uchaguzi wa tawi na kusimikwa kuwa mwenyekiti wa tawi bokorani lililopo kata ya mtoni wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam kwa kipindi cha miaka mitano Awali mwenyekiti huyo aliwahi kuwa kada wa chadema na kiongozi mkuu ngazi ya Wilaya Temeke kwa sababu zenye mashiko aliamua kuachana na chama cha CHADEMA na kujiunga na chama tawala CCM Mwenyekiti JOSEPH YONA alisema kuna wapinzani wanacheka mimi kuwa mwenyekiti wa ccm ngazi ya tawi kwa kile wanachoona ni kushuka kisiasa lakini nataka kuwaambia mchakato wa kumpata mwenyekiti wa tawi ndani ya chama cha mapinduzi ni mgumu kuliko ule mchakato wa kumpata mwenyekiti wa chadema ngazi ya taifa Aliongeza na kusema kuwa mwenyekiti wa tawi ccm anahadhi kuliko mwenyekiti wa Taifa chadema Pia alitoa msimamo wake kuwa hana mpango wa kusogea ngazi ya mkoa wala taifa kwani katika matawi ndio kuna wanachama wanao takiwa kusaidiwa hivyo aliomba asisumbuliwe sumbuliwe yeye ni Mwenyekiti wa tawi na anataka kukaa tawini Aliwaomba wanachama wa chama cha mapinduzi na wananchi wote kwa ujumla kulaani vikali baadhi ya vyombo vya habari vinavyo toa taarifa ya kupandikiza chuki baina ya serikali na wananchi, taarifa za uchochezi hivyo alianzisha oparetion CCM KARIBU NYUMBANI WANANCHI TUSOME UHURU Aliyazungumza hayo siku ya kuwaaga wanachama wa chama cha mapinduzi Tawi la michungwani kiembe samaki lililopo Tanzinia visiwani ambalo lilifanya ziara ya siku tano katika tawa la ccm bokorani hii ni kwaajiri ya kudumisha muungano By Albert Personal assistance

DataTz Group Tech

DataTz Group Tech
Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea BLOG, WEBSITE, LOGO, PHONE APP, vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762 Asante na Karibu Sana.