CCM TAWI LA BOKORANI

Hapa ni nyumbani kwetu wote

MWENYEKITI WA TAWI

Kiongozi bora kwa ustawi wa tawi

TAWI LA WANANCHI WOTE

Tawi ni watu na watu ndo sisi

MWENYEKITI WA TAWI

Kiongozi bora kwa ustawi wa tawi

TAWI LA WANANCHI WOTE

Tawi ni watu na watu ndo sisi

TANZANIA YETU

Magufuli kwa maendeleo

Thursday, 21 September 2017

UCHAGUZI UWT NGAZI YA WILAYA LEO, KATIBU MKUU MAKILAGI ASISITIZA TARATIBU ZIZINGATIWE

DAR ES SALAAM
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Amina Makillagi, amewataka wagombea na wajumbe wote wa mikutano mikuu ya wilaya kwenye Uchaguzi wa jumuiya hiyo ngazi ya wilaya utakaofanyika leo, tarehe 21/9/2017 kuzingatia maadili ya Chama na UWT.

 "Kubwa ni kutotoa wala kupokea rushwa. UWT imejiandaa vizuri kuhakikisha inafuatilia nyendo zozote ovu zitakazojitokeza katika Uchaguzi. Mgombea yeyote atakayetoa rushwa atachukuliwa hatua za kinidhamu kabla na baada ya Uchaguzi kuisha ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nafasi ya uongozi iliyopatikana kwa mazingira tatanishi", amesema Makilagi. 

Makillagi ambaye amewatakia uchaguzi mwema wanachama wote wa UWT, amesisitiza kuwa rushwa haitavumilika na kwa mjumbe yeyote atakayepokea rushwa na kwamba kanuni zilizopo zitamuwajibisha ipasavyo.

Friday, 15 September 2017

CCM YAMPONGEZA ALIYE KODI NDEGE YA KUMSAFIRISHA LISSU KENYA

Chama cha mapinduzi kimempongeza mbunge na mwanachama mwenzao Salim Hassan Turyk Mbunge wa jimbo la mpendae kwakuonyesha utu na ukomavu wa kisiasa na upendo kwa mwanasiasa na mwanasheria wa chama cha chadema Tundu Lissu baada ya kuvamiwa na watu wasio julikana wakiwa na sira
Mbunge huyo alitoa udhamini kwaajiri ya kupatikana ndege ya kumpeleka Lissu kenya kwaajiri ya matibabu
Aidha chama kupitia polepole wamesema Mbunge huyo ni mfano wa kuigwa kunako mattzo basi tofauti za kisiasa zikae pembeni  utu na ubinadamu uchukue nafasi

Thursday, 14 September 2017

JOSEPH YONA AWAONYA CHADEMA

*CHADEMA WEKENI AKIBA YA MANENO*

Kupitia ukurasa wake WA facebook Joseph Yona mwenyekiti ccm yawi La bokorani 

Hili tamko la Lema ukiliangalia *objectively* ni moja kati ya *Matamko ya Hovyo* kuwahi kutokea baada ya shambulio la Mh. Tundu Lisu. *Sitaki kuamini* kwamba tamko hilo lina *Baraka za chama*

Wote tunakubaliana sote kwamba tukio lililotokea ni *ovu na lakusikitisha* lakini tukio hili lisitumike vibaya katika kutafuta *sympathy na umaarufu wa kisiasa* in a wrong way. Ni *mpuuzi tu* ndiye anaweza kumbebesha spika (as an individual)  mzigo wa lawama kutokana na kilichotokea kwa Mh. Lisu.

1. *Kuhusu Bunge kuahirisha shughuli zooote* - Lema alitaka shughuli zote za Bunge ziahirishwe

- Je, jambo hilo ni la kufanywa na Ndugai AS an individual?

- Yupo Mbunge yeyote wa ukawa *aliyejaribu* kutoa hoja hiyo ikakakataliwa au kupuuzwa?

2. *Kuhusu Bunge kujadili ulinzi wa wabunge* toka majumbani kwao

- Hivi practically nchi hii inahitaji ulinzi kwa wabunge *zaidi* kuliko kwa watu wengine?

- Na kama mpaka sasa Chadema imeonesha wazi *kutokuwa na imani* na vyombo vya ulinzi na usalama vya Serikali Lema alitaka Bunge lifikie  *azimio gani* katika jambo hili kwamba kila Mbunge apewe askari (asiyeaminika) ili amlinde 24/7 au?

3. Lema anamlaumu spika kwa *kuwaita kwenye kamati Mh. Kubenea na Zzk*

- Anajua hasa wameitiwa nini?

- Anaudanganya umma kwamba Kubenea ameitwa kwasababu ya kutaja utofauti wa idadi ya risasi kwahiyo Chadema imekubaliana kutumia tukio hili *kumshambulia spika* kwamba ni *muongo*?

- Maana idadi ya risasi zilizosemwa na Spika alinukuu kwamba ni kwa mujibu wa RPC sasa *tumuunge mkono* Kubenea kwa kusimama madhabahuni na kusema " *spika amedanganya umma risasi alizopogwa ni 38 na si 32*" ?

- Lema hajui kwamba kilichokuwa kikisemwa ni makisio tu, anakumbuka press ya kwanza ya Mbowe alisema Lisu amepigwa risasi ngapi?

- Zitto *kama ana hoja* kuhusu *ukiukwaji wa kanuni za Bunge* kwa kitendo cha kamati za Bunge (Almas na Tanzanite)  kuwasilisha ripoti zao nje ya Bunge kwanini asipeleke hoja hiyo bungeni...Spika ndugai Uliposhika shikilia hapo hapo usiteteleke hata kidogo..watanzania wazalendo tunakuunga mkono..

Nawasilisha ni YONA mkiti wa CCM tawi la bokorani

Sunday, 10 September 2017

ESTER BULAYA AKAMATWE MARA MOJA

TUNAOMBA AKAMATWE MARA MOJA
Mwanasiasa na mbunge wa cha CHADEMA Ester amos bulaya ameamsha hisia za wanasiasa wengi pamoja na wananchi wapenda amani na mshikamano bila kujali itikadi za kisiasa kutokana na kile alicho kiandika katika ukurasa wake na kutukana jeshi la police kwa kuwaita WAPUMBAVU.

Mwenyekiti wa ccm tawi la bokorani JOSEPH YONA amesema vyombo vyetu vya ulinzi vinatakiwa viheshimike haiwezekani mtu apate ujasiri wa kulitukana jeshi la polisi NO HAIKUBARIKI 

Rais JPM aliagiza vyombo vyetu vya ulinzi viheshimike hili la mwanasiasa huyu halikubaliki mbali nakutukana ameingilia kazi za kipolisi ni utaratbu na wajibu wa polisi kumu hoji yeyote watakae ili kukamilisha kazi zao ikiwa dereva wa lissu ndo mtu pekee alikuwa na mbunge mpaka tukio linatokea huoni anaweza kusaidia maelezo ya awali kuhusu tukio hilo sasa what bad kama wakimuhitaji 

Nitapoteza imani na jeshi langu pendwa kama mbunge huyu hato chukuliwa hatua ili kulinda hadhi ya jeshi letu 

Alisema mwenyekiti huyo wa chama cha mapinduzi tawi la bokorani ambae amekuwa kuwa kiongozi wa chini katika chama lakini mwenye mitazamo chanya juu ya kulijenga taifa na chama kwa ujumla

Saturday, 9 September 2017

DEREVA WA LISSU ATAKIWA KITUONI DODOMA

RPC MUROTO amesema kuwa dereva wa mwanasheria na mwanasiasa wa chama cha chadema ambaye alishambuliwa na risasi juzi nyumbani kwake dodoma na watu wasio julikana amesema dereva w TUNDU LISSU ametoweka dodoma bila taarifa hivyo tuna mtaka awasili katika kituo cha police mkoa wa dodoma ili kuhakikisha zoezi la upelelezi juu ya shambulio hilo

   Alisema kuwa tunasikitishwa kuona dereva wa lissu hatki kutoa ushirikiano juu ya police na kumtaka afike mara moja alisisitza kuwa nimemuona akihojiwa na gazeti la mtanzania saa anashindwaje kuja kuisaidia jeshi la police

Akimaliza kwa kuwa taka wananchi kuwa wapole na kuzuia mihemko yao juu ya tukio la mwanasiasa huyo Sisi tupo tumekula kiapo cha uweridi tutafanya hivyo bila tatzo ila kama jeshi la urizi wa raia na mali zake hatuta fumbia macho kwa wale wote watakako vunja utaratibu so kwahili la lissu yote ifike sehm ashauriki

Friday, 8 September 2017

IGP SIRRO AWATAKA WAJISALIMISHE


IGP SIRRO amewakata wale wote walio tajwa kwenye report ya madini ya Tanzanaite na dhahabu iliyo kabidhiwa jana katika ikulu ya magogoni awata wajisalimishe sababu majarada yao tayari yamesha funguliwa kwa kutimiza majukumu yao ya kuwahoji na kufanya uchunguzi ili kuubaini ukweli


Aidha ametumia fulsa hiyo kuufahamisha Umma kuwa hali ya amani ndani ya tanzania ni shwari kabisa na kuahidi kushirikiana na wanachi ili kuhakikisha kuwa wale wote walio husika na kushambuliwa kwa tundu lissu wanapatikana na sheria itafwata mkondo wake


Pia Sirro amesema watachukuliwa hatua za kisheria wale wote wanao onyesha kufurahishwa na tukio la kushambuliwa kwa mwanasiasa na  mwanasheria wa CHADEMA

BY.


JOSEPH YONA

Wednesday, 6 September 2017

MANGULA AWASHA MOTO DAR

MANGULA AZUNGUMZA NA WENYEVITI WA MASHINA KINONDONI, ASEMA WASALITI WALIWABEBA WAPINZANI DAR

  Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara, Philip Mangula akizungumza na Wenyeviti wapya wa Mashina ya CCM waliochaguliwa katika uchaguzi ndani ya Chama, uliofanyika hivi karibuni, alipokutana nao leo katika Ukumbi wa Vijana Sodial Hall, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.Picha:Bashir Nkoromo.
------------------
Na Bashir Nkoromo
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara Philip  Mangula, amesema wapinzani hawakuwa na uwezo wa kushinda katika baadhi ya majimbo na kata  jijini Dar es Salaam, katika uchaguzi mkuu uliopita isipokuwa walisaidiwa na wasaliti ndani ya chama.

Amesema, kutokana na madhara hayo, CCM itaendelea kuwasaka na kuwang'oa wasaliti hao, wakiwemo wale waliofanikiwa kujipenyeza na kushinda nafasi mbalimbali katika uchaguzi ndani ya Chama CCM na ndiyo maana CCM imefuta uchaguzi kwenye baadhi ya kata.

Mangula amesema hayo leo katika kikao chake na Wenyeviti wapya wa Mashina ya CCM, kutoka kata za Kawe na Kinondoni, waliochaguliwa hivi karibuni, kilichofanyika leo Vijana Social Hall, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amesema, tayari chama kimeshachukua hatua mbalimbali kwa wasaliti kuanzia ngazi ya taifa, mikoa na kata kwa kuwapa adhabu zikiwemo za kuwafuta uanachama, onyo kali na wengine kuendelea kuchunguzwa.

"japokuwa tumekwishachukua hatua mbalimbali dhidi ya wasaliti lakini bado kazi hii inaendelea hadi tuhakikishe tabia hii chafu ya usaliti inakoma ndani ya chama, kwa sababu ni jambo la kushangaza CCM yenye wanachama wengi kiasi hiki kuliko chama chochote inapoteza majimbo katika mazingira yasiyo na majibu", alisema Mangula.

Akitoa tathimini kuhusiana na wasaliti ngazi ya mkoa, alisema jumla ya viongozi 4595 walikuwa wasaliti ndani ya Chama walipewa onyo, huku 3907 wapo chini ya uangalizi wa miezi 12.

Wengine waliopewa kalipio ya miezi 18 walikuwa 4, wengine 398 wapo katika uchunguzi, 465 wameadhibiwa, huku waliofukuzwa na kuvuliwa uwanachama wapo 2267.

Mangula aliwataka Wenyeviti hao wapya kuwa mstari wa mbele kuhakikisha CCM inaimarika katika maeneo yao kwa kuzingatia misingi na kanuni ambayo mojawapo ni kuepuka kupokea na kutoa rushwa hasa nyakati za uchaguzi.

Akimkaribisha mangula kuzungumza na wenyeviti hao, katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe aliwataka watendaji katika matawi yenye miradi kuisimamia kwa makini midari hiyo hasa upande wa mapato, ili mapato yanayopatikana yatumike pia kuwalipa japo kidogo wenyeviti wa mashina.

DataTz Group Tech

DataTz Group Tech
Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea BLOG, WEBSITE, LOGO, PHONE APP, vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762 Asante na Karibu Sana.