Saturday, 5 August 2017

ALICHO KISEMA JOSEPH YONA JUU YA SERIKALI YA JPM

YA AWAMU YA TANO NI HAPA KAZI TU SI NGUVU YA SODA WASANII WATAUMBUKA.
Kwa haki ya moyo wangu, ninayo furaha isiyo kifani ambayo haielezeki, tokea serikali ya awamu ya tano iingie madarakani.
Tokea Rais wa awamu ya tano Dr. Joseph Magufuli aingie madarakani, sisi ambao tunayo mapenzi makubwa na nchi yetu kwa dhati kabisa,Rais anatufariji na tumeamua kusahau shida zetu kwani Tanzania yenye neema tunaiona.
Leo hii makundi ya watu katika Taifa hili ni mijadala mikali kuhusu serikali ya Dr.Magufuli. Ukitaka uondoke na manundu wakati wa mjadala,jaribu kumponda Dr. Mangufuli. Maumivu makubwa waliyokuwa wakiyapata watu wa hali ya chini kiuchumi,yanapona baada ya kumpata Daktari bigwa wa shida zetu Rais Dr. Joseph Magufuli.
Wakati natafakari namna bora ya kufikisha ujumbe huu, joto na homa kali ya mijadala kuhusu Magufuli inaendelea,kwenye vijiwe,vyuo,mashuleni,majumbani,mahosipitalini,daladala na maneno mengine,hata majeshini.
Wakati nachukua kalamu yangu kuanza kuandika liliniijia wazo la kujadili Makanikia lakini baadae nikaona ni vizuri niliache kwani viongozi wetu walikuwa kwenye kikao cha majadiliano na kampuni ya Barrick Gold.
Harakati za Magufuli zimenirudisha nyuma sana ili nitafute pesa kwa udi na uvumba niweze kusoma historia ya aliyewahi kuwa Rais wa Jamhuri ya watu wa china Deng Xiao ping.
Natamani nimsome Deng Xiao Ping harakati zake kwenye utawala wake, baada ya mkutano mkuu wa chama cha kikomunisti cha china,miaka ya 1978 kutafakari Taifa lao na kuona ni namna gani wapate mtu wa mabadaliko.
Ndipo kwa kauli moja mkutano huo mkuu ukampa Deng Xiao Ping kulisukuma gurudumu la maendeleo ya watu wa china, na ukweli ni kuwa Deng Xiao Ping hakuwaangusha wachina.
Leo hii chama cha mapinduzi,baada ya tafakari sana Dodoma,walifanikiwa kumpata Deng Xiao Ping wa Tanzania ambaye ni Dr. Joseph Magufuli.
Binafsi kuna vitu vidogo tu ambavyo Dr. Magufulli kaanza navyo na anaendelea,naamini Rais Dr. Joseph Magufuli hatatuangusha watanzania.
Kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu,Magufuli unatufariji watanzania, sana tena sana.
Zamani Marais walikuwa wakiwabembeleza wabunge kwa posho, sasa wewe endelea na harakati zako, watanzania wote bila itikadi tunaungana pamoja katika safari yako ya kutuletea maendeleo.
Ni kweli watanzania wa kawaida wamekuelewa,kuwa uchaguzi umekwisha kila mmoja kwa nafasi yake afanye kazi ili kulikomboa Taifa , kila mmoja awajibike
Mimi binafsi wakati wa kampeni kwa dhati rais alikuwa anaongelea matatizo yanayoigusa jamii ya chini, aliyokuwa akiongea yaliyotoka moyoni mwake kabisa.
Bahati nzuri wakati wa kampeni, nilifanikiwa kupata bahati ya kuwa msemaji msaidizi wa kampeni za aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la moshi mjini CCM, Devis Mosha.
Kwa kweli Dr. Magufuli alivyokuwa anaongelea shida za Moshi,Mkoa wa Kilimanjaro, na kanda nzima ya kaskazini aliongea mambo ambayo yapo na watu wa Mikoa hiyo na ushabiki wao wa kupanua vidole badala ya kupanua akili, walisema jamaa anajua kila kitu.
Binafsi kwa miaka kumi na tatu nikiwa upinzani kabla ya kujiunga na CCM, nilichojifunza kuwa upinzani ni  usanii, ujanja ujanja , uhuni nk,walau kwa ujio wa ACT-wazalendo.
Ni vyama ambavyo wapiga dili ni wengi sana tukiyafumua madudu yao ni aibu, hata kupewa udiwani,ila kwa vile 2015 ulikuwa uchaguzi wa simba na yanga (ushabiki) tumshukuru Mungu kwa haki kutupatia changuo sahihi ambalo watanzania walikuwa wanalisubiria.Leo barabarani pita na nguo ya CCM unafurahiwa na kuitwa “hapa kazi tu”.
Na leo kwa dhati kabisa nakumbuka msemo unaosema kabla hujafa mwenyezi mungu atakuumbua tuu.
Leo  ujio wa Dr. Joseph Magufuli unaenda kuwaumbua chadema,kwani walizoea usanii,ujanja ujanja ,uhuni.Pia nilishasema hakuna kiongozi chadema,nikatukanwa nikabezwa, nikatekwa, nikatupwa, nikafa kwa kudra za Mungu nikafufuka ili niweze kushuhudia wanavyoumbuliwa duniani.
Chadema ilikuwa ikisubiri,CCM wakosee ili ipitie hapo hapo, nikasema kuna ombwe la uongozi Chadema nikabezwa,nikasema Zitto yuko sahihi hataki usanii,nikafukuzwa kazi,leo kabla jogoo hajawika Dr. Magufuli kaondoa ajenda zao zote za usanii kilichobaki ni kazi tu.
Chadema kabla ya kuingia ikulu walianzisha michakato/mikakati mitano, leo nitaitaja kwa kifupi ila nitakuja kuielezea kwa kirefu mbeleni. Mkakati wa kwanza Operation sangara,hii ilianzia kanda ziwa na ilitakiwa isambae kanda zote Tanzania bara walipanga kanda kumi, visiwani mbili. Mkakati huu ulilenga kuitukana CCM kuwa ni sangara (samaki pandikizi) wao chadema samaki wazaliwa, hivyo ilikuwa ni kuichonganisha CCM na wananchi, nilimhoji Mbowe na wewe ni sangara una mahoteli nje na makampuni yanayokwepa kodi,na amedhulumu NHC jingo lao.
Nikamwambia Mbowe mbele ya viongozi wa chadema dar-es-salaam enzi hizo kwa sasa naona wana nyadhifa kubwa kwa mfano meya wa ubungo na wa jiji.
Mkakati wa pili,huu ulikuwa ni mkakati wa kuteka watu wenye umaarufu nchini kama vile viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wanafunzi,wafanyabiashara,wanasiasa nk. Mkakati huu ulilenga kuwachonganisha raia na CCM kuwa ndio wauwaji, watekaji nk ili chadema wapate umaarufu,huu ulikuwa mkakati wa siri wa ofisi ya mwenyekiti Taifa.Na mkakati huu uliandaliwa vyombo vya habari kama Mwanahalisi,Tanzania daima n.k kuichafua ccm.
Mkakati wa tatu ulikuwa ni Movement for change(M4C), ndani ya mkakati huu ilikuwa ni kufanya mikutano mikubwa na midogo na kuanzisha chadema ni msingi. Kuwa chama kiende mpaka ngazi ya chini,baada ya mikakati ya kwanza ya kuichonganisha CCM. Pia mkakati huu ulichangiwa na Kornad Adenuer Stifftung(KAS) ya ujerumani, wadau, mitandao ya simu, michango nk. Na ndani ya mkakati huu mchakato wa katiba mpya iwekwe,migomo wampotezee mwelekeo Rais,wamsifie mwenyekiti wa tume alewe sifa wapite katikati.
Mkakati wa nne, ulikuwa ni delete/ondoa CCM, mkakati huu pia ulikuwa umeandaliwa gharama na mahelkopita kibao na yatengewe mabendera na vipeperushi vingi vibandikwe barabarani kabla ya uchaguzi mkuu, pia ndani yake itengenezwe mikakati ya kujijeruhi kwenye mikutano ionekane ni CCM.
Mkakati wa mwisho ni uchaguzi mkuu hapa kwa haraka haraka pamoja na mambo mengine, mabango na mabendera yawe mengi.Kitu ambacho namshukuru Mungu mikakati yao mingi ilishindikana, kwani kuna mikakati mingine iliingilia kati mfano vua gamba, kuunda ukawa, kufukuzana,kuitana wasaliti na uimara wa komredi katibu mkuu wa ccm Kinana.Kinana uliiweka ccm imara na yale yote uliyokuwa ukiyapigania,serikali ya awamu ya tano inatekeleza.Naamini ninayoyaandika kwenye makala hii,kuonesha ni namna gani Obwe la Uongozi onekani tarajiwa la chadema wajue, tulisema tuko huru.
Rais Dr. Joseph Mangufuli tupia macho na vyuo vikuu wizi wa ununuzi wa chemical za maabara na vifaa,huko napo pesa zake zinaweza jenga barabara na vifaa vya hospitalini.
Ukweli ni kuwa vyama vya upinzani,niliwaambia viongozi wake kuwa ccm inabadilika kulingana na wakati,leo kwa Rais huyu,wapinzani mtaisoma namba,ccm mbele kwa mbele.
Mwisho viongozi baadhi wa serikali katika kipindi hiki nuhimu na adimu ambapo Rais wetu analitafakari Taifa kwa kina, ninaomba baadhi yenu acheni usanii na ujanja ujanja.
Rais Dr. Joseph Magufuli kwa kauli mbiu yake ya “hapa kazi tu” anamanisha na yanatoka moyoni.                                           Ni Joseph Yona
0713-802226 .

0 comments:

Post a Comment

DataTz Group Tech

DataTz Group Tech
Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea BLOG, WEBSITE, LOGO, PHONE APP, vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762 Asante na Karibu Sana.