CCM TAWI LA BOKORANI

Hapa ni nyumbani kwetu wote

MWENYEKITI WA TAWI

Kiongozi bora kwa ustawi wa tawi

TAWI LA WANANCHI WOTE

Tawi ni watu na watu ndo sisi

MWENYEKITI WA TAWI

Kiongozi bora kwa ustawi wa tawi

TAWI LA WANANCHI WOTE

Tawi ni watu na watu ndo sisi

TANZANIA YETU

Magufuli kwa maendeleo

Saturday, 5 August 2017

FURSA KUBWA KWA WA TANZANIA

:::::::::BOMBA LA MAFUTA NI FURSA KWA WATANZANIA::::::::::

👉Naungana na mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Magufuli na Serikali yake pamoja na Rais Mseveni wa Uganda kwa kuandika historia mpya ya ushirikiano wenye tija.

👉Historia inaandikwa kwa nchi mbili za Tanzania na Uganda ambapo jiwe la msingi linawekwa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani bandari ya Tanga nchini Tanzania ambapo jiwe la msingi la kuanza ujenzi huo litawekwa.

👉Ni heshima Kubwa nchi yetu ya Tanzania kupata fursa hii ya bomba la mafuta kupita nchini Tanzania ambao utapita mikoa 8, Wilaya 24 na vijiji 184.

👉Kuna faida nyingi sana kama Taifa tutapata kutokana na uwepo wa mradi huu wa bomba la mafuta.

👉Wakati wa ujenzi Watanzania wengi watapata fursa ya ajira ambapo jumla ya ajira 40,000 zitapatika. Ajira za ufundi, ulinzi, upishi, usafiri, fursa za malazi, na huduma za kifedha.

👉Ukiachilia mbali fursa hiyo mradi huu utapelekea kufunguka kwa Ukanda wa Biashara kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki kama vile Rwanda, Burundi, Kongo, Sudan ambapo wanaweza kuunganishwa na miundombinu hiyo na kusafirisha mafuta kwa urahisi.

👉Kukamilika kwa mradi huo nchi za Tanzania na Uganda zitapata mapato na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wake.

👉Faida nyingine ya bomba la mafuta kuwa ni pamoja na gharama za mafuta kupungua kutokana na nchi za Afrika Mashariki kutumia mafuta yake yenyewe kwenye magari pamoja na ndege hivyo kuchochea kasi ya utalii katika nchi husika pamoja na ajira.

👉Gharama ya mafuta itakapo pungua ni dhahiri gharama za usafiri, usafirishaji na bidhaa nazo pia zitapungua. Maisha kuwa rahisi.

👉Naipongeza Serikali ya Dk. Magufuli kwa kufanikisha upatikanaji wa ujenzi huu wa bomba la mafuta kutoka Uganda. Haikuwa kazi rahisi Tanzania kupata fursa hii ya bomba la mafuta kutoka nchini Uganda kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo.

👉Narudia tena kumpongeza Dk. Magufuli kwa kutuletea mradi huu wa bomba la mafuta utakaokuwa na tija kwa Taifa vizazi na vizazi. Ni jukumu letu Watanzania kuulinda mradi huu wa bomba la mafuta.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Dk. Magufuli

Nawasilisha ni YONA mkiti wa CCM tawi la bokorani

ALICHO KISEMA JOSEPH YONA JUU YA SERIKALI YA JPM

YA AWAMU YA TANO NI HAPA KAZI TU SI NGUVU YA SODA WASANII WATAUMBUKA.
Kwa haki ya moyo wangu, ninayo furaha isiyo kifani ambayo haielezeki, tokea serikali ya awamu ya tano iingie madarakani.
Tokea Rais wa awamu ya tano Dr. Joseph Magufuli aingie madarakani, sisi ambao tunayo mapenzi makubwa na nchi yetu kwa dhati kabisa,Rais anatufariji na tumeamua kusahau shida zetu kwani Tanzania yenye neema tunaiona.
Leo hii makundi ya watu katika Taifa hili ni mijadala mikali kuhusu serikali ya Dr.Magufuli. Ukitaka uondoke na manundu wakati wa mjadala,jaribu kumponda Dr. Mangufuli. Maumivu makubwa waliyokuwa wakiyapata watu wa hali ya chini kiuchumi,yanapona baada ya kumpata Daktari bigwa wa shida zetu Rais Dr. Joseph Magufuli.
Wakati natafakari namna bora ya kufikisha ujumbe huu, joto na homa kali ya mijadala kuhusu Magufuli inaendelea,kwenye vijiwe,vyuo,mashuleni,majumbani,mahosipitalini,daladala na maneno mengine,hata majeshini.
Wakati nachukua kalamu yangu kuanza kuandika liliniijia wazo la kujadili Makanikia lakini baadae nikaona ni vizuri niliache kwani viongozi wetu walikuwa kwenye kikao cha majadiliano na kampuni ya Barrick Gold.
Harakati za Magufuli zimenirudisha nyuma sana ili nitafute pesa kwa udi na uvumba niweze kusoma historia ya aliyewahi kuwa Rais wa Jamhuri ya watu wa china Deng Xiao ping.
Natamani nimsome Deng Xiao Ping harakati zake kwenye utawala wake, baada ya mkutano mkuu wa chama cha kikomunisti cha china,miaka ya 1978 kutafakari Taifa lao na kuona ni namna gani wapate mtu wa mabadaliko.
Ndipo kwa kauli moja mkutano huo mkuu ukampa Deng Xiao Ping kulisukuma gurudumu la maendeleo ya watu wa china, na ukweli ni kuwa Deng Xiao Ping hakuwaangusha wachina.
Leo hii chama cha mapinduzi,baada ya tafakari sana Dodoma,walifanikiwa kumpata Deng Xiao Ping wa Tanzania ambaye ni Dr. Joseph Magufuli.
Binafsi kuna vitu vidogo tu ambavyo Dr. Magufulli kaanza navyo na anaendelea,naamini Rais Dr. Joseph Magufuli hatatuangusha watanzania.
Kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu,Magufuli unatufariji watanzania, sana tena sana.
Zamani Marais walikuwa wakiwabembeleza wabunge kwa posho, sasa wewe endelea na harakati zako, watanzania wote bila itikadi tunaungana pamoja katika safari yako ya kutuletea maendeleo.
Ni kweli watanzania wa kawaida wamekuelewa,kuwa uchaguzi umekwisha kila mmoja kwa nafasi yake afanye kazi ili kulikomboa Taifa , kila mmoja awajibike
Mimi binafsi wakati wa kampeni kwa dhati rais alikuwa anaongelea matatizo yanayoigusa jamii ya chini, aliyokuwa akiongea yaliyotoka moyoni mwake kabisa.
Bahati nzuri wakati wa kampeni, nilifanikiwa kupata bahati ya kuwa msemaji msaidizi wa kampeni za aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la moshi mjini CCM, Devis Mosha.
Kwa kweli Dr. Magufuli alivyokuwa anaongelea shida za Moshi,Mkoa wa Kilimanjaro, na kanda nzima ya kaskazini aliongea mambo ambayo yapo na watu wa Mikoa hiyo na ushabiki wao wa kupanua vidole badala ya kupanua akili, walisema jamaa anajua kila kitu.
Binafsi kwa miaka kumi na tatu nikiwa upinzani kabla ya kujiunga na CCM, nilichojifunza kuwa upinzani ni  usanii, ujanja ujanja , uhuni nk,walau kwa ujio wa ACT-wazalendo.
Ni vyama ambavyo wapiga dili ni wengi sana tukiyafumua madudu yao ni aibu, hata kupewa udiwani,ila kwa vile 2015 ulikuwa uchaguzi wa simba na yanga (ushabiki) tumshukuru Mungu kwa haki kutupatia changuo sahihi ambalo watanzania walikuwa wanalisubiria.Leo barabarani pita na nguo ya CCM unafurahiwa na kuitwa “hapa kazi tu”.
Na leo kwa dhati kabisa nakumbuka msemo unaosema kabla hujafa mwenyezi mungu atakuumbua tuu.
Leo  ujio wa Dr. Joseph Magufuli unaenda kuwaumbua chadema,kwani walizoea usanii,ujanja ujanja ,uhuni.Pia nilishasema hakuna kiongozi chadema,nikatukanwa nikabezwa, nikatekwa, nikatupwa, nikafa kwa kudra za Mungu nikafufuka ili niweze kushuhudia wanavyoumbuliwa duniani.
Chadema ilikuwa ikisubiri,CCM wakosee ili ipitie hapo hapo, nikasema kuna ombwe la uongozi Chadema nikabezwa,nikasema Zitto yuko sahihi hataki usanii,nikafukuzwa kazi,leo kabla jogoo hajawika Dr. Magufuli kaondoa ajenda zao zote za usanii kilichobaki ni kazi tu.
Chadema kabla ya kuingia ikulu walianzisha michakato/mikakati mitano, leo nitaitaja kwa kifupi ila nitakuja kuielezea kwa kirefu mbeleni. Mkakati wa kwanza Operation sangara,hii ilianzia kanda ziwa na ilitakiwa isambae kanda zote Tanzania bara walipanga kanda kumi, visiwani mbili. Mkakati huu ulilenga kuitukana CCM kuwa ni sangara (samaki pandikizi) wao chadema samaki wazaliwa, hivyo ilikuwa ni kuichonganisha CCM na wananchi, nilimhoji Mbowe na wewe ni sangara una mahoteli nje na makampuni yanayokwepa kodi,na amedhulumu NHC jingo lao.
Nikamwambia Mbowe mbele ya viongozi wa chadema dar-es-salaam enzi hizo kwa sasa naona wana nyadhifa kubwa kwa mfano meya wa ubungo na wa jiji.
Mkakati wa pili,huu ulikuwa ni mkakati wa kuteka watu wenye umaarufu nchini kama vile viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wanafunzi,wafanyabiashara,wanasiasa nk. Mkakati huu ulilenga kuwachonganisha raia na CCM kuwa ndio wauwaji, watekaji nk ili chadema wapate umaarufu,huu ulikuwa mkakati wa siri wa ofisi ya mwenyekiti Taifa.Na mkakati huu uliandaliwa vyombo vya habari kama Mwanahalisi,Tanzania daima n.k kuichafua ccm.
Mkakati wa tatu ulikuwa ni Movement for change(M4C), ndani ya mkakati huu ilikuwa ni kufanya mikutano mikubwa na midogo na kuanzisha chadema ni msingi. Kuwa chama kiende mpaka ngazi ya chini,baada ya mikakati ya kwanza ya kuichonganisha CCM. Pia mkakati huu ulichangiwa na Kornad Adenuer Stifftung(KAS) ya ujerumani, wadau, mitandao ya simu, michango nk. Na ndani ya mkakati huu mchakato wa katiba mpya iwekwe,migomo wampotezee mwelekeo Rais,wamsifie mwenyekiti wa tume alewe sifa wapite katikati.
Mkakati wa nne, ulikuwa ni delete/ondoa CCM, mkakati huu pia ulikuwa umeandaliwa gharama na mahelkopita kibao na yatengewe mabendera na vipeperushi vingi vibandikwe barabarani kabla ya uchaguzi mkuu, pia ndani yake itengenezwe mikakati ya kujijeruhi kwenye mikutano ionekane ni CCM.
Mkakati wa mwisho ni uchaguzi mkuu hapa kwa haraka haraka pamoja na mambo mengine, mabango na mabendera yawe mengi.Kitu ambacho namshukuru Mungu mikakati yao mingi ilishindikana, kwani kuna mikakati mingine iliingilia kati mfano vua gamba, kuunda ukawa, kufukuzana,kuitana wasaliti na uimara wa komredi katibu mkuu wa ccm Kinana.Kinana uliiweka ccm imara na yale yote uliyokuwa ukiyapigania,serikali ya awamu ya tano inatekeleza.Naamini ninayoyaandika kwenye makala hii,kuonesha ni namna gani Obwe la Uongozi onekani tarajiwa la chadema wajue, tulisema tuko huru.
Rais Dr. Joseph Mangufuli tupia macho na vyuo vikuu wizi wa ununuzi wa chemical za maabara na vifaa,huko napo pesa zake zinaweza jenga barabara na vifaa vya hospitalini.
Ukweli ni kuwa vyama vya upinzani,niliwaambia viongozi wake kuwa ccm inabadilika kulingana na wakati,leo kwa Rais huyu,wapinzani mtaisoma namba,ccm mbele kwa mbele.
Mwisho viongozi baadhi wa serikali katika kipindi hiki nuhimu na adimu ambapo Rais wetu analitafakari Taifa kwa kina, ninaomba baadhi yenu acheni usanii na ujanja ujanja.
Rais Dr. Joseph Magufuli kwa kauli mbiu yake ya “hapa kazi tu” anamanisha na yanatoka moyoni.                                           Ni Joseph Yona
0713-802226 .

Thursday, 3 August 2017

CCM YAPAZA SAUTI


TANZANIA PRIME MINISTER PROMISE NEW JOBS

(PM) Kassim Majaliwa has promised cheap, reliable grid power to support new jobs for Tanzanians.

In the comments below, tell him how getting access to reliable and cheap grid power would change your life.

Tuesday, 1 August 2017

CHADEMA WANAUPUNGUFU WA WATAALAMU KWA KIASI KIKUBWA

CHADEMA INA UPUNGUFU WA WATAALAMU KWA KIASI KIKUBWA.

Na Thadei Ole Mushi.

#Toka juzi tumesikia kuwa Kamati kuu ya CHADEMA imekutana kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayolihusu Taifa. Hawa wameitana nchi nzima wakaja kulipana posho baada ya hapo wakatoa uharo wakaondoka zao.

Nimeshtushwa na tamko au maazimio ya kamati kuu leo ambapo kamati kuu imetoa maoni yao kama ifuatavyo:-

1.Tumekuwa tunafanya uchumi wa matukio, kurukia rukia matukio Makinia limezikwa, tupo kweye Tegeta Escrow na IPTL  - Mbowe

#MBOWE na kamati kuu ina maana hawaoni hatua zinazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa Escrow? Ina maana alitaka swala la makenikia limalizike siku ile ile? Ina maana haoni wala kusikia kuwa wameshakuja kwa ajili ya majadiliano.

#Kama kamati kuu wangepaswa kutoa plan B ya namna ya kushughulikia swala hilo kama Serikali ilikurupuka. Kilichowakwamisha ni kukosa wataalamu wa kutoa hiyo plan B.

2. Kama wabunge wa pande zote mbili wangekuwa na msimamo hii bajeti ya serikali ya 2017/2018 isingepita - Mbowe

#Hajatuambia mapungufu ya Budget yenyewe, tulisikia wakiichangia na michango yao ilichukuliwa na kuwekwa kwenye budget husika. Kama kuna mapungufu walipewa fursa ya kuyasemea ndani ya Bunge huku njee anatuambia ili tufanyeje? Kweli naamini jamaa aligonga ziro form Six...

3.Fedha zililizopelekwa kununua ndege zingepelekwa kwenye kilimo kuna Watanzania zaidi ya milioni 40 wangecheka' - Mbowe

#Akili ya wapi hii? Huwezi kuniambia kuwa ndege hizo zina hasara tu na hazina faida. Kila kiongozi ana priority zake mbona yeye hurusha chopa nchi nzima badala ya kujenga ofisi ya chama? Angelipaswa kutupa mchanganuo wa hasara ya kununua hizo ndege na faida ya kuwekeza kwenye kilimo. Alipaswa kuita wataalamu wa chama watueleze kwa data kuwa fedha hizo zingefanya nini kwenye kilimo na faida yake na baadaye watuambie kutokana na kunua ndege tumepoteza kiasi gani cha fedha. Ile ziro ya Six hakusingiziwa ni yake kabisa.

4.Viongozi wetu wa Serikali walio wengi hawajui A, B, C za uchumi - Mbowe

#Yeye na Ziro yake ya Six anajua uchumi gani? Ni nani pale Chadema anayeju uchumi? Ni lema? Au sugu? Ni silinde? Au mnyika? Ni lisu au yeye mbowe? Labda ni lowasa aliyeshindwa kujua ni hasara kiasi gani taifa lingepata kwa kuwapa tenda Richmond au ni Sumaye aliyeiuza NBC Kwa bei ya noah? Mbowe akili zipo sawa kweli?

5.Wawekezaji wa ndani wamekuwa waoga kufanya uwekezaji ndani ya nchi kwa kuwa wanahofia kesho anaweza kuibuka mtu akasema vunja hapa - Mbowe

#Uwekezaji upi anaouzungumzi huyu jamaa ni ule wa kuyokulipa kodi pale NHC? Kuna atakayehoji tena kwa nn alifeli six? Yeye alikuwa mfano wa mwekezaji kwa kuwekeza jengo la NHC akairusha serikali kodi na baadaye akataka kufoji nyaraka achukue na jengo kabisa.

6.Siku kadhaa kabla ya bajeti kupitishwa wabunge wa chama fulani walipewa milioni kumi kumi ili wapitishe bajeti - Mbowe

#Hakuna chama kinachoitwa chama fulani.... kama ana uhakika aseme ni chama gani na awapeleke mahakamani.

#Kwa maana hiyo kujifungia kote na kulipana Posho ni ujinga huu mnakuja kutueleza?

Chadema mna haja ya kuwekeza kwa wataalamu mnapwaya kwa kuwa hakuna wataalamu wa kuwasaidia kufanya analysis ya mambo mbali mbali. Ni kweli kuwa labda fedha za Bombadier zingewekezwa kwenye kilimo zingeleta tija ila how? hapo ndio mlitakiwa kujikita na serikali kweli ingeshtuka.

#Au labda kwa kujenga reli ya Standard Gauge kuelekea Moro kusingekuwa na tija kama kuwekeza kwenye kilimo.... mngechukua kiasi cha fedha ambazo zingetumika kujenga Reli hiyo halafu muangalie kwa kwenda Moro kuna tija gani halafu mseme labda fedha hiyo ingetumika kufanya ABCD.... Au Reli hiyo ingeelekezwa sehemu fulani kwa kuwa kuna ABCD.... nimewapa mfano hapo.

Nendeni pale UDSM mkatafute vijana wa UCHUMI wawasaidie halafu mje na critical thinking si kupiga soga hapo kijiweni Ufipani halafu mtuletee hizi hekaya.

Ole Mushi

DataTz Group Tech

DataTz Group Tech
Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea BLOG, WEBSITE, LOGO, PHONE APP, vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762 Asante na Karibu Sana.